Monday, August 9, 2010

YATOKANAYO NA KIKAO:

kumekucha wajumbe.. ni siku nyingine tena aliyoifanya Mungu imempendeza tuione baada ya wikiend nzuri iliyokuwa na kila aina ya bashasha na Baraka tele makofi mengi-mengi basi!!!!!

ndugu wajumbe, jana tullifanya kikao kama tulivyokuwa tumeazimia na agenda kubwa na kuu ilikuwa ni kujadili na kutengeneza katiba ambayo itatuongoza katika kuendesha kikundi chetu kwa weledi mkubwa.

WAJUMBE WALIOHUDHURIA KIKAO:
MOSES MSEMO
STEWART CHILOLO
RUMISHA META
KISEKEMI EPHRAIM
SILVANUS CHANGWA
JOHN NKUNGU
GOODLUCK MURO
LUCKFORD DIDAS


kikao kilienda vizuri kila mjumbe akionyesha utulivu katika kuhakikisha kwamba malengo ya kuwa na katiba bora yanafikiwa ipasavyo.

tulifanikiwa kuitengeneza katiba huku Katibu akipewa jukumu la kwenda kuichapa na kuja nakala za kutosha za wajumbe wote ili tuifanyie uhakiki wa mwisho kabla ya kuipa  katiba mamlaka ili ituongoze. 

KIKAO KIJACHO NI TAREHE 15/08.2010;

Nawasilisha.



No comments: